Lyrics

Lava Lava – Desh Desh Lyrics

Lava Lava Desh Desh Lyrics

Mola kamuumba
Hana mfano weee! !
Mzuri wa sura na roho
Na njema tabia iyaaa
Unyagoni kafundwa
Kwa makungwi somo weee!!
Mahaba yajaza ndoo
Yanimwagikia iyaaa
Nataman nimtaje hata jina
Ila naficha naficha
Naifanya siri yangu
Kina fulan wale wakusigina
Mkaleta mapicha mapicha
Akatoroka ndege wangu

Si mrefu Si mfupi (ah eh)
Si mweupe Si mweusi (ah eh)
Rangi yake ni ya katikati
Kasema kwangu afurukuti (ah eh)
Kwengine anaogopa nuksi (ah eh)
Mi ni wake milele haniachi ndo maana
Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja ( Nan)
Amenifika kwa roho makopakopa (kopaa)
Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja (Nani)
Iila umtaja ooh naogopa ogopa
Kwa jina namuhifadhi

Desh Desh, Desh Desh
Msije kuninyakulia
Desh Desh deeeesh!!!! kipenzi changu jamani
Desh Desh, Desh Desh
Mkaja kuniharibia
Desh Desh deeeesh!
Penzi likawa mashakani
Nananaa! Nna Nna!
Nananaa! Nna Nna!
Nananaa! Nna Nna!

Najua najua
Roho zinawauma
Hampendi kuona mwenzenu na nawiri
Najua mwenzenu najua
Mwakesha kujituma
Kutwa kwa masangoma yangu kuyatabir
Mliosema nimeachika
Hainifiki mikosi
Mola ndo mpaji
Nyongo mtazitapika
Mchomwe jua la utosi
Kesheni kunijaji

Mwenzenu kila kukicha
Kabla kupewa misosi
Masaji masaji
Tunavyowakasirisha
Yani hata tukiposti
Hataki nimtagi
Enhe si mtu wamagazeti
Wala page za udaku ilo mkae mkijua
Hataki taki eeeh
Mambo yake ssiri yeti
Poleni washakunaku
Wala msijisumbue
Kumsachi Sachi

Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja (Nani)
Amenifika kwa roho
Makopakopa kopaa (kopa)
Nampenda mpenda (Nani)
Kijana mmoja (Nani)
Ila kumtaja ooh naogopa ogopa
Kwa jina namuhifadhi

Desh Desh, Desh Desh deeeesh
Msije kuninyakulia
Desh Desh deeeesh ! !!
Kipenzi changu jamani
Desh Desh, Desh Desh
Mkaja kuniharibia
Desh Desh deeeesh!
Penzi likawa mashakani
Nananaa! Nna Nna! !
Nananaa! Nna Nna!
Nananaa! Nna Nna!

 

  • Written by: Lava Lava
  • Album: Desh Desh
  • Released: 2022
  • Official Video:

Leave a Response